Jumamosi 28 Juni 2025 - 09:19
Wazayuni waomba fidia kutoka kwa Netanyahu

Hawza/ Televisheni ya Israel imeripoti kupokea maelfu ya maombi ya fidia kutoka kwa Wazayuni baada ya kumalizika kwa vita na Iran na kutokana na uharibifu mkubwa uliosalia katika maeneo ya kati ya ardhi inayokaliwa kwa mabavu.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza Televisheni ya Israel imetangaza kuwa imepokea maelfu ya maombi ya fidia kutoka kwa Wazayuni baada ya kumalizika kwa vita na Iran na kutokana na hasara kubwa iliyosababishwa katika sehemu ya kati ya ardhi inayokaliwa kwa mabavu.

Kituo cha Televisheni cha Israel cha "Channel 13" kimeripoti kuwa, licha ya kutangazwa kwa usitishaji wa mapigano, serikali ya Israel baada ya vita na Iran inakabiliana na changamoto nyingi za kiuchumi na za miji.

Katika muendelezo wa ripoti hiyo imeelezwa kuwa gharama ya uharibifu uliotokea katika ardhi zilizokaliwa kwa mabavu imefikia mabilioni ya "shekeli" kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa. Vilevile, maelfu ya maombi ya fidia yamewasilishwa kwa taasisi za utawala wa Israel.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Tel Aviv na maeneo ya kati yamepata madhara makubwa zaidi, na Mamlaka ya Ushuru ya Israel imepokea maombi ya fidia 25,000 hadi sasa. Hadi sasa, ni thuluthi moja tu ya maombi haya ndiyo yaliyoshughulikiwa, na tathmini kamili ya uharibifu inatarajiwa kuchukua wiki kadhaa kukamilika.

Tanbihi: "Shekeli" ni sarafu rasmi ya Israel.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha